Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Balozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, amesisitiza kuwa Iran haitawahi kusalimu amri mbele ya vitisho, mashinikizo wala vitendo vya kutisha kutoka kwa mataifa ya nje.
Akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Iravani alisema Iran imeazimia kuendelea kulinda mamlaka yake ya kitaifa, usalama wa nchi na wananchi wake, huku akisisitiza kuwa Tehran haijawahi kujadiliana chini ya vitisho na haitawahi kukubali kushinikizwa.
Aidha, aliitaka Marekani kuachana na sera za vitisho vya kijeshi na kutumia njia ya mazungumzo yenye kuheshimu usawa wa mataifa na sheria za kimataifa ikiwa kweli inataka suluhisho la kidiplomasia.
Iravani aliongeza kuwa Iran itaendelea kutetea haki na maslahi yake halali, akisisitiza kuwa mashinikizo ya kisiasa, kijeshi au kiuchumi hayataifanya Jamhuri ya Kiislamu kuachana na misimamo yake ya msingi.
Your Comment